Jumatano 11 Februari 2026 - 03:30
Haram ya Hadhrat Abbas (a.s.) yaonesha vipande vya kale vya haram hii tukufu

Hawza/ Makumbusho ya Haram ya Hadhrat Abbas (a.s) yameonesha vipande vya kale na vya kihistoria vya haram ya Qamar Bani Hashim ambavyo viliharibiwa katika tukio la mwaka 1370 (H).

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mkusanyiko huu pia unajumuisha vipande vitatu vya mawe ya marumaru vinavyoonesha hati ya usanifu wa jengo, ambavyo vilikuwa vimewekwa juu ya iwan ya dhahabu ya uwanja wa haram tukufu, na vinaanzia katika zama za Sultani Abdulhamid wa Pili wa Dola ya Uthmani.

Maelezo ya kipande cha kwanza cha marumaru yana michoro ya rangi na mapambo ya maua pamoja na sahihi ya Sultani Abdulhamid Khan. Kipande hiki kinahesabiwa kuwa nyaraka ya kihistoria, ambacho kilipata uharibifu mkubwa wakati wa Intifadha ya Shaaban, jambo lililosababisha kazi hiyo kugawanyika vipande vipande.

Vipande vya pili na vya tatu ni mawe mawili ya marumaru yaliyowekwa katika iwan ya dhahabu kwenye mlango wa kuingia katika haram tukufu. Mawe haya kwa hakika ni mabamba mawili yenye maandishi kwa hati ya Kiosmani, yaliyotekelezwa kwa mtindo wa nakshi iliyoinuliwa, na yanajumuisha mkusanyiko wa beti za mashairi ambazo huenda ziliandikwa kwa ajili ya kumsifu Hadhrat Abal-Fadhli Abbas (a.s.).

Mkuu wa Idara ya Masuala ya Utamaduni katika Haram ya Hadhrat Abbas (a.s.), Bwana Nafiʿ al-Mousawi, amesema kuhusiana na jambo hili: “Athari hizi za kihistoria zinaonesha kumbukumbu yenye sura mbili; kwa upande mmoja zinarekodi hatua muhimu ya historia ya ukarabati wa Ataba Tukufu, na kwa upande mwingine zinatukumbusha mashambulizi ya kinyama dhidi ya urithi wa kidini katika Intifadha ya Shaaban.”

Aliongeza kuwa: “Vipande hivi vitatu vinaonesha hati kamili na vinakumbusha maumivu ya historia ya kisasa ya Iraq yaliyotokea katika siku za mwezi wa Shaaban, wakati mkono wa dhulma na ukandamizaji ulipofikia urithi wetu wa kidini na wa thamani. Bado kuna mashahidi hai watasimulia simulizi ya dhulma hiyo katika vizazi vijavyo.”

Chanzo: Al-Kafeel

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha